As-Salamu Alaykum
Moja ya amali nzuri katika Uislamu ni kutafuta elimu. Katika Qur’ani Tukugu Mwenyezi Mungu ameanza kumhutubu mwanadamu kwa maneno ya “Kusoma”, “Elimu” na “Kitabu.” Hii ni kwa sababu elimu ni njia ya kufikia saada na ukamilifu wa mwanadamu. Mwanadamu kwa kutumia elimu, anaweza kuainisha mustakbali autakao yeye. Mara zote Mtume Mtukufu (saw) na masahaba zake, walikuwa wakihimiza sana kusoma. Katika mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu imenukuliwa kuwa, baada ya vita vya Badr kila mateka ambaye alikuwa akiwafundisha kusoma na kuandika wakazi 10 wa mji wa Madina, alikuwa akiachiliwa huru. Suala hilo ni ushahidi tosha na wa wazi juu ya uzingatiaji mkubwa wa dini ya Kiislamu na Mtume Muhammad (saw) kuhusiana na elimu na utafutaji wake kwa ujumla. Mtukufu huyo alikuwa akiipa umuhimu mkubwa kila aina ya elimu kama vile alivyomtaka mmoja wa masahaba zake kujifunza lugha ya Kisyriac. Mtume Mtukufu (saw) amepokelewa akisema, “Tafuteni elimu hata kama ni kutoka China.” Hadithi hiyo kama zilivyo hadithi nyinginezo, inasisitizia umuhimu wa elimu katika Uislamu. Sisitizo na ushawishi huo, kuhusiana na elimu, ndivyo vimewafanya Waislamu kutilia umuhimu na kufanya juhudi kubwa za kutafua elimu duniani. Mbali na hayo Waislamu walikuwa wakitarjumu kila athari yoyote ya kielimu waliyoipata. Kwa utaratibu huo, licha ya kwamba, Waislamu waliunda mfumo wa mahusiano kati ya tamaduni za Ugiriki, Urumi, Misri, India na nyinginezo, waliweza pia kuibua utamaduni na ustaarabu muhimu katika historia ya mwanadamu, uliokuja kufahamika kwa jina la “Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu.”
Dini Tukufu ya Kiislamu iwe ni katika maandiko yake au kwa upande wa mwenendo wake wa kihistoria haina mkinzano wowote ule, bali tangu mwanzoni mwa kudhihiri kwake ilitoa amri ya watu kutafuta elimu, kiasi kwamba, sehemu kubwa ya aya na riwaya za kidini imezingatia zaidi suala la elimu na umuhimu wake na kubainisha thamani ya mtu aliye na elimu. Kwa hakika nafasi ya elimu katika Uislamu ni muhimu mno na ina daraja ya faradhi ya kidini. Hii ni kwa sababu hakuna mipaka katika kutafuta elimu. Kwa mtazamo wa Uislamu elimu zote ambazo zina faida kwa mwanadamu, zinapaswa kusomwa na watu. Kuhusiana na hilo Mtukufu Mtume (saw) anasema, “elimu ni zaidi ya kile ambacho kinaweza kuhesabika, basi chukua kile kilicho bora.” Kwa mujibu wa wa riwaya hiyo, Uislamu haukubana elimu katika fani fulani tu, bali umewataka wafuasi wake kujifunza na kutafuta elimu zote ambazo zina manufaa kwa mwanadamu. Kimsingi ni kuwa, Waislamu wanaamini kwamba, kadiri mtu anavyokuwa na elimu kubwa, ndivyo maarifa yake kwa Mwenyezi Mungu yanavyokuwa mengi. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa fikra ya Kiislamu, elimu na dini ni mambo mawili yanayoambatana kikamilifu. Katika Uislamu elimu yenye manufaa imesisitizwa sana. Aidha kwa mtazamo wa Uislamu, elimu haina maana ya elimu ya kidini au elimu ambayo ina manufaa kwa Akhera tu hapana, bali kusudio la elimu yenye manufaa ni elimu ambayo ina manufaa kwa mwanadamu kwa njia moja au nyingine, yawe ni ya kimaada au ya kimaanawi.
Neno ‘Darajaat’ yaani daraja, lililotumika katika aya hii na lenye maana 'mutlaki' yaani bila kuainisha kiwango hasa cha daraja hiyo, katika lugha ya Qur'ani linabainisha adhama na ukubwa. Yaani kwa lugha nyingine ni daraja za juu. Katika kufasiri aya hii tukufu, Sahaba Abudhar al-Ghaffari amenukuliwa akisema kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia: Ewe Abudhar, Mwenyezi Mungu, malaika na mitume wake wanampenda Twalibul-ilmi, yaani mtu anayetafuta elimu. Na elimu haipendwi ila na mtu mwenye saada, hivyo ni furaha gani atakayokuwa nayo mtu mwenye kutafuta elimu siku ya Kiama. Na mtu yeyote anayetoka nyumbani kwake kwa ajili ya kujifunza mlango mmoja wa elimu, basi Mwenyezi Mungu atamuandikia malipo kwa kila hatua atakayoipiga sawa na thawabu za mmoja wa mashahidi wa vita vya Badr. Na mtafutaji wa elimu ni kipenzi wa Mwenyezi Mungu na mtu yeyote atakayekuwa na mapenzi na elimu, basi pepo ni mali yake. Na atakuwa katika radhi za Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni na hatoondoka duniani isipokuwa atanyweshwa katika Haudh ya Kauthar. Kisha atakula matunda ya peponi na akiwa peponi atakuwa rafiki wa Hadhrati Khidhri (as).” Katika hadithi nyingine Mtume Mtukufu anasema: “Siku ya Kiama, wakati mtu mwenye elimu na mchaji-Mungu watakuwa kwenye Swiratw, yaani njia nyembamba, mchaji-Mungu ataambiwa, aingie peponi na afurahie matunda ya ibada yake aliyoifanya duniani. Na mtu mwenye elimu ataambiwa; bakia hapa na umuombee shufaa mtu au rafiki yeyote umtakaye, kwani kila yeyote utakayemuombea basi dua yako atakubaliwa. Hivyo yule mtu mwenye elimu atasimama katika kisimamo cha Mitume na kuwaombea marafiki na watu wake wa karibu ili wasamehewe dhambi zao. Kwani siku ya Kiama makundi matatu ndiyo yatakayokuwa na hadhi ya kufanya maombezi yaani shufaa, makundi hayo ni Mitume, wasomi na mashahidi.” Mwisho wa hadithi.
Moja ya amali nzuri katika Uislamu ni kutafuta elimu. Katika Qur’ani Tukugu Mwenyezi Mungu ameanza kumhutubu mwanadamu kwa maneno ya “Kusoma”, “Elimu” na “Kitabu.” Hii ni kwa sababu elimu ni njia ya kufikia saada na ukamilifu wa mwanadamu. Mwanadamu kwa kutumia elimu, anaweza kuainisha mustakbali autakao yeye. Mara zote Mtume Mtukufu (saw) na masahaba zake, walikuwa wakihimiza sana kusoma. Katika mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu imenukuliwa kuwa, baada ya vita vya Badr kila mateka ambaye alikuwa akiwafundisha kusoma na kuandika wakazi 10 wa mji wa Madina, alikuwa akiachiliwa huru. Suala hilo ni ushahidi tosha na wa wazi juu ya uzingatiaji mkubwa wa dini ya Kiislamu na Mtume Muhammad (saw) kuhusiana na elimu na utafutaji wake kwa ujumla. Mtukufu huyo alikuwa akiipa umuhimu mkubwa kila aina ya elimu kama vile alivyomtaka mmoja wa masahaba zake kujifunza lugha ya Kisyriac. Mtume Mtukufu (saw) amepokelewa akisema, “Tafuteni elimu hata kama ni kutoka China.” Hadithi hiyo kama zilivyo hadithi nyinginezo, inasisitizia umuhimu wa elimu katika Uislamu. Sisitizo na ushawishi huo, kuhusiana na elimu, ndivyo vimewafanya Waislamu kutilia umuhimu na kufanya juhudi kubwa za kutafua elimu duniani. Mbali na hayo Waislamu walikuwa wakitarjumu kila athari yoyote ya kielimu waliyoipata. Kwa utaratibu huo, licha ya kwamba, Waislamu waliunda mfumo wa mahusiano kati ya tamaduni za Ugiriki, Urumi, Misri, India na nyinginezo, waliweza pia kuibua utamaduni na ustaarabu muhimu katika historia ya mwanadamu, uliokuja kufahamika kwa jina la “Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu.”
************************************
Kwa mujibu wa mtazamo wa Waislamu, elimu na dini ni vitu viwili
visivyotengana, bali ni vitu vinavyoenda sambamba. Kadhalika taaluma
mbalimbali za kielimu kama vile fizikia, nyota, elimu ya ardhi, elimu ya
tiba, hesabu na mithili ya hizo, zilikuwa zikifundishwa katika vituo
vya kielimu vya Waislamu. Aidha mbali na hayo, Waislamu waliasisi
maktaba kubwa tofauti katika vituo vya kielimu na kidini na hivyo
kuifanya elimu na dini kuwa vitu viwili vinavyohitajiana. Hii ni katika
hali ambayo uelewa finyu wa viongozi wa Kikristo kuhusiana na uhusiano
wa dini na elimu, ulipelekea historia ya Ulaya kugawanyika katika zama
mbili za kipindi cha imani na kipindi cha elimu, huku wakiifanya elimu
kukabiliana na imani. Katika Karne za Kati, mitazamo ya kielimu na
kifalsafa, ilikuwa ikitolewa tu na kanisa na hakuna msomi yeyote
aliyekuwa na haki ya kutoa nadharia yake ya kielimu kinyume na mtazamo
rasmi wa kanisa, kiasi kwamba, nadharia ya kielimu iliyokwenda kinyume
na mtazamo wa kanisa, ilionekana kuwa ni sawa na kukufuru na kumpinga
Mungu. Kwa msingi huo wasomi waliokuwa wakitoa mitazamo iliyopingana na
mitazamo rasmi ya kanisa walikuwa wakifungwa jela, kuhukumiwa kifo au
kuteketezwa motoni.
*************************************
Dini Tukufu ya Kiislamu iwe ni katika maandiko yake au kwa upande wa mwenendo wake wa kihistoria haina mkinzano wowote ule, bali tangu mwanzoni mwa kudhihiri kwake ilitoa amri ya watu kutafuta elimu, kiasi kwamba, sehemu kubwa ya aya na riwaya za kidini imezingatia zaidi suala la elimu na umuhimu wake na kubainisha thamani ya mtu aliye na elimu. Kwa hakika nafasi ya elimu katika Uislamu ni muhimu mno na ina daraja ya faradhi ya kidini. Hii ni kwa sababu hakuna mipaka katika kutafuta elimu. Kwa mtazamo wa Uislamu elimu zote ambazo zina faida kwa mwanadamu, zinapaswa kusomwa na watu. Kuhusiana na hilo Mtukufu Mtume (saw) anasema, “elimu ni zaidi ya kile ambacho kinaweza kuhesabika, basi chukua kile kilicho bora.” Kwa mujibu wa wa riwaya hiyo, Uislamu haukubana elimu katika fani fulani tu, bali umewataka wafuasi wake kujifunza na kutafuta elimu zote ambazo zina manufaa kwa mwanadamu. Kimsingi ni kuwa, Waislamu wanaamini kwamba, kadiri mtu anavyokuwa na elimu kubwa, ndivyo maarifa yake kwa Mwenyezi Mungu yanavyokuwa mengi. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa fikra ya Kiislamu, elimu na dini ni mambo mawili yanayoambatana kikamilifu. Katika Uislamu elimu yenye manufaa imesisitizwa sana. Aidha kwa mtazamo wa Uislamu, elimu haina maana ya elimu ya kidini au elimu ambayo ina manufaa kwa Akhera tu hapana, bali kusudio la elimu yenye manufaa ni elimu ambayo ina manufaa kwa mwanadamu kwa njia moja au nyingine, yawe ni ya kimaada au ya kimaanawi.
*****************************************
Katika aya ya 11 ya Surat al-Mujaadala, Mwenyezi Mungu anaelezea
umuhimu wa elimu na daraja ya juu waliyonayo maulama na wasomi mbele ya
watu wengine kwa kusema: "Mwenyezi Mungu anawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu."Neno ‘Darajaat’ yaani daraja, lililotumika katika aya hii na lenye maana 'mutlaki' yaani bila kuainisha kiwango hasa cha daraja hiyo, katika lugha ya Qur'ani linabainisha adhama na ukubwa. Yaani kwa lugha nyingine ni daraja za juu. Katika kufasiri aya hii tukufu, Sahaba Abudhar al-Ghaffari amenukuliwa akisema kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia: Ewe Abudhar, Mwenyezi Mungu, malaika na mitume wake wanampenda Twalibul-ilmi, yaani mtu anayetafuta elimu. Na elimu haipendwi ila na mtu mwenye saada, hivyo ni furaha gani atakayokuwa nayo mtu mwenye kutafuta elimu siku ya Kiama. Na mtu yeyote anayetoka nyumbani kwake kwa ajili ya kujifunza mlango mmoja wa elimu, basi Mwenyezi Mungu atamuandikia malipo kwa kila hatua atakayoipiga sawa na thawabu za mmoja wa mashahidi wa vita vya Badr. Na mtafutaji wa elimu ni kipenzi wa Mwenyezi Mungu na mtu yeyote atakayekuwa na mapenzi na elimu, basi pepo ni mali yake. Na atakuwa katika radhi za Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni na hatoondoka duniani isipokuwa atanyweshwa katika Haudh ya Kauthar. Kisha atakula matunda ya peponi na akiwa peponi atakuwa rafiki wa Hadhrati Khidhri (as).” Katika hadithi nyingine Mtume Mtukufu anasema: “Siku ya Kiama, wakati mtu mwenye elimu na mchaji-Mungu watakuwa kwenye Swiratw, yaani njia nyembamba, mchaji-Mungu ataambiwa, aingie peponi na afurahie matunda ya ibada yake aliyoifanya duniani. Na mtu mwenye elimu ataambiwa; bakia hapa na umuombee shufaa mtu au rafiki yeyote umtakaye, kwani kila yeyote utakayemuombea basi dua yako atakubaliwa. Hivyo yule mtu mwenye elimu atasimama katika kisimamo cha Mitume na kuwaombea marafiki na watu wake wa karibu ili wasamehewe dhambi zao. Kwani siku ya Kiama makundi matatu ndiyo yatakayokuwa na hadhi ya kufanya maombezi yaani shufaa, makundi hayo ni Mitume, wasomi na mashahidi.” Mwisho wa hadithi.
*****************************************
Katika hadithi za Ahlubayti wa Mtume (as) pia umesisitizwa umuhimu wa
kutafuta elimu. Mtume (saw) anasema: “Kujifunza elimu ni faradhi kwa
kila Muislamu.” Hatua ya kusisitizwa sana elimu na kufikia daraja ya
ulazima wa kidini, inaonyesha ni kiasi gani Uislamu unavyotilia umuhimu
suala zima la elimu na kupambana na ujinga. Mbali na hayo Mtume anasema:
“Tambueni kuwa, Mwenyezi Mungu anampenda mtu anayetafuta elimu yoyote
ile.” Maneno haya ya Mtukufu Mtume (saw) yanaonyesha kuwa, elimu haina
kiwango wala mpaka bali elimu haiwezi kuwa na mwisho. Kwa ajili hiyo
ikiwa mtu atajifunza elimu kwa kiwango chochote, basi atakuwa katika
radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini wale wanaofanya juhudi zaidi
katika njia hiyo, kwa hakika watakuwa wenye kupendwa zaidi. Kuhusiana na
suala hilo Sayyid Muhammad Hussein Twabatwabai msomi na mfasiri mkubwa
wa Qur’ani Tukufu anatafsiri aya ya 9 ya Surat Zumarnayosema: “Je
afanyaye ibada wakati wa usiku kwa kusujudu na kusimama na kuogopa
Akhera na kutarajia rehema za Mola wake…. (ni sawa na asiyefanya hayo)?
Sema: Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?
Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” Allamah Twabatwabai
anaamini kuwa, katika aya hiyo suala la kuwa na elimu na kutokuwa na
elimu kwa pamoja limetajwa katika namna ya mutlaqi. Lakini madhumuni
yake ni elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu, kwa kuwa elimu hiyo ndiyo
inayomfikisha mwanadamu kwenye ukamilifu na ndio uhalisia wa neno
manufaa. Aidha kutokuwa na elimu hiyo kunamsababishia mwanadamu madhara
makubwa. Lakini elimu nyinginezo, ni kama mali na utajiri ambazo manufaa
yake ni kwa ajili ya maisha ya humu duniani na ni zenye kuishia hapa
hapa duniani. Hivyo hadi sasa tuna makundi mawili ya wasomi, msomi
muuminina msomi asiye muumini. Kundi la kwanza ndilo linalopendekezwa
zaidi na ndilo pia lililo bora. Kadhalika Mwenyezi Mungu anasema: “Soma
kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba Mwanadamu katika pande la
damu. Soma na Mola wako ni Mtukufu mno. Ambaye amefunza (kuandika) kwa
kalamu. Amemfunza mwananadamu asilolijua.” Surat Alaq aya ya
1-5. Katika aya hizi kumetajwa daraja na hadhi ya uepo wa mwanadamu.
Daraja bora zaidi ya mwanadamu ni ile ya mtu aliyesoma na kuelimika.
WABILLAHI TAUFIQ
No comments:
Post a Comment