ASSALAM ALAYKUM WARAHMATU LLAHI WABARAKATUH
Jumuiya ya wanafunzi kiislamu wa Teofilo Kisanji ambayo ipo chini ya Tamsya Mkoa wa Mbeya, leo tarehe 08/01/2017 imepata viongozi wapya katika ngazi mbalimbali za jumuiya hiyo. Viongozi hao walitangazwa na Katibu mkuu wa Tamsya wa Mkoa wa Mbeya na baadae kuridhiwa na wanajumuiya wote ambao walihudhuria katika hafla hiyo. Miongoni mwa viongozi walioteuliwa walikuwa ni kama ifuatavyo:
Amir wa jumuiya: Adnan Imran
Amirat wa jumuiya: Tatu Amour
Viongozi wengine ni manaibu Amir na Amirat wa jumuiya, makatibu wa jumuiya, pia maamiri na makatibu wa idara mbalimbali za jumuiya ikiwemo idara ya uchumi, idara ya habari na mawasiliano, idara ya elimu, idara ya daa'wa na maadili pamoja na idara nyenginezo.
Tunamuomba Allah (sw) amfanyie wepesi Amir wetu mpya katika kuiongoza jumuiya hii pamoja na viongozi wengine wanaomsaidia ili kufikia malengo ya jumuiya pamoja na kuipeleka mbele dini yetu ya uislam.
Amiiin yaa rabbala alamin
ReplyDelete